Description
Kitabu hiki kinachunguza vipengele vya kimsingi vya ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili (L2). Baadhi ya yale yaliyoshughulikiwa ni: Lugha, Nadharia za Ufundishaji wa Lugha ya Pili, Uandalizi wa somo, Tathmini, Sera ya Lugha ya Kiswahili, Mbinu za Kufundishia, Nyenzo za Kufundishia, Kufundisha Masuala Ibuka kwa Kiswahili, Stadi ya Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma, Kuandika pamoja na Sarufi na Matumizi ya Lugha. Kitabu hiki ni kielelezo kifaacho kwa walimu wanaofundisha Kiswahili na wanafunzi wa kiswahili katika vyuo. Kinazingatia kwa kina yaliyomo katika silabasi za viwango mbalimbali na kupendekeza njia na mbinu zinazoweza kutumika wakati wa kufundisha.
Dkt. Rachel Koross ni mwalimu mwenye uzoefu na tajriba katika ufundishaji wa Kiswahili. Ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Eldoret (UOE) kitivo cha Elimu. Ana shahada za B.Ed (Chuo Kikuu cha Moi), Uzamili (Chuo Kikuu cha Moi) na Uzamifu (Chuo Kikuu cha Moi). Amefundisha Kiswahili katika vyuo kadhaa na shule ya upili. Ameandika pia kitabu ‘Enhancing National Unity in Kenya: The use of oral literature in Kiswahili’ na makala mbalimbali katika majarida.
Dkt. Felicity Murunga ni msomi na mwandishi mwenye tajriba iliyokolea. Hivi sasa ni mhadhiri katika kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Eldoret (UoE). Ana shahada za B.Ed (Chuo Kikuu cha Egerton), Uzamili (Chuo Kikuu cha Moi) na Uzamifu (Chuo Kikuu cha Moi). Baadhi ya vitabu vyake ni Mwongozo wa Utengano na Dafina ya Fasihi Simulizi: Vipera na Ufundishaji wake.
Reviews
There are no reviews yet.