Mitindo ya Lugha ya Kidijitali katika Facebook

Category:

Description

Uvumbuzi wa teknolojia ya intaneti umesababisha kuzuka kwa lugha mpya katika mitandao, ambayo sasa inarejelewa kama lugha ya kidijitali. Kitabu hiki kinajadili mitindo mbalimbali ya kimawasiliano inayotambulisha lugha ya kidijitali katika mtandao wa Facebook. Katika kufanya hivi, kitabu kinabainisha sababu ambazo zimechangia kuibuka kwa lugha hii na kufafanua matatizo ya kimawasiliano yanayotokana na matumizi ya mitindo anuwai ya kimawasiliano katika Facebook. Kitabu hiki, kadhalika, kimeangaza kwa kina ruwaza za lugha ya kidijitali na kubainisha kategoria za mitindo yenyewe.

Kitabu cha Mahero Toboso Bernard ni cha kiwango cha juu. Mwandishi ametoa mchango mkubwa sana katika kudhihirisha mitindo ya lugha kidijitali katika Facebook. Kitabu hiki pia ni cha kipekee kwa sababu kimeshughulikia sababu zinazosababisha kuibuka kwa mitindo ya lugha ya kidijitali katika jamii. Kitabu hiki kimechapishwa kwa wakati mzuri ambapo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeshika kani katika jamii. Aghalabu, vijana wanaotumia Facebook katika mawasiliano yao. Pia, hivi sasa nchini Kenya, asasi za serikali zimeanza kutumia Facebook kama mojawapo ya njia za kuwasiliana na wananchi wa kawaida mashinani. Kitabu hiki kitawafaa wahadhiri, walimu na wanafunzi wa lugha na Isimujamii katika viwango mbalimbali za elimu [Dkt. Dave Bowen; Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Kabarak, Kenya].

Dkt Toboso Mahero Bernard ni mwenyekiti wa Idara ya Lugha na Elimu ya Fasihi katika Chuo Kikuu Kishirikishi cha Alupe. Ana shahada katika B.Ed kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta na shahada za Uzamili na Uzamifu kutoka Chuo Kikuu cha Moi. Dkt Toboso ana tajiriba kubwa katika ufundishaji wa lugha na fasihi.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Mitindo ya Lugha ya Kidijitali katika Facebook”

Your email address will not be published. Required fields are marked *