Kurunzi ya Sarufi ya Kiswahili – Shule za Upili

Category:

Description

Kitabu hiki kimeandikwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtaala mpya unaolenga umilisi wa lugha kwa njia sahihi na yenye mvuto ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kulingana na maelekezo ya Wizara ya Elimu. Kitabu hiki vile vile kimeshugulikia mada mbalimbali kwa namna ambayo kitamwezesha mwanafunzi kuelewa kikamilifu mada husika. Mada zote zinahusu sarufi kwa shule za upili kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne. Mada hizi zimeshugulikiwa kwa uangalifu na kwa umakinifu ili kumjenga mwanafunzi kwa kumpa nafasi ya umilisi wa lugha ya Kiswahili. Kuna mifano na mazoezi anuawi zitakazomwezesha mwalimu kupima umilisi wa mwanafunzi kutoka katika mada mbali mbali za lugha. Mbinu mbali mbali zimetumika kama vile mifano na kujadili hoja. Mbinu hizi zitamsaidia mwanafunzi kuelewa mada kwa njia rahisi zaidi.

 

Erick Ochieng ni kasisi wa kanisa katoliki na pia mwalimu wa shule za upili. Amehitimu na shahada ya elimu katika somo la dini na kiswahili. Amefunza somo la kiswahili kwa miaka mingi. Fauka ya hayo ana tajriba, maarifa na ujuzi wa kufunza sarufi katika kiwango hiki cha shule za upili na mwisho ameshiriki katika warsha za Kiswahili kiwango cha kitaifa.

 

 

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kurunzi ya Sarufi ya Kiswahili – Shule za Upili”

Your email address will not be published. Required fields are marked *