Dafina ya Fasihi Simulizi: Vipera na Mbinu za Ufundishaji

Category:

Description

Dafina ya Fasihi Simulizi ni kitabu kinachochunguza vipengele vya kimsingi vya fasihi simulizi. Vipengele vifuatavyo vimezingatiwa kwa kina: Dhana ya fasihi simulizi, Maana na sifa za tanzu za fasihi simulizi, Utafiti nyanjani, Ufundishaji wa fasihi simulizi na Nadharia za ufndishaji wa lugha ya pili. Kitabu hiki kitawafaidi wanafunzi, walimu, watafiti, na wapenzi wa lugha ya Kiswahili ili waweze kuelewa na kufurahia fasihi simulizi. Kitabu hiki ni tunu kwa wanafunzi na walimu katika kila daraja: shule za msingi, za upili, na hata vyuo vikuu. Hii ni DAFINA kuu kwa wapenzi wa lugha na fasihi kwa Kiswahili.

Dkt. F. Murunga ni mwenye tajriba pana katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za upili na vyuo vikuu. Pia ameandika Mwongozo wa Utengano.

Dkt David Wamamili Wanyonyi ni mwalimu mwenye tajriba katika lugha na fasihi ya Kiswahili. Amewahi kufundisha Kiswahili katika shule za Obera (Nyanza Kusini) na Sikusi (Bungoma). Kwa sasa ni mhadhiri katika kitivo cha elimu, Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret.

Bw. A.K. Biwott ni mwalimu wa lugha ya Kiswahili katika shule ya upili. Hivi sasa anashughulikia shahada yake ya
uzamili (MA) katika kitivo cha Sanaa na Sayansi Jamii, Chuo Kikuu cha Moi.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Dafina ya Fasihi Simulizi: Vipera na Mbinu za Ufundishaji”

Your email address will not be published. Required fields are marked *