Mofofonolojia Linganishi ya Lahaja za Kimaasai: Kenya na Tanzania

(1 customer review)

Category:

Description

Mofofonolojia Linganishi ya Lahaja za Wamaasai – Kenya na Tanzania ni kazi ya kwanza kabisa kuchanganua lahaja za Kimaasai kwa misingi ya kisayansi. Ni kazi inayochanganua isimu ya lugha mojawapo ya Kiafrika na kufikia viwango vya kimataifa kama kazi zingine tajika za Katamba (1989), Lass (1984) na Mathews (1974). Lugha ya Kimaasai ina wingi wa lahaja zilizo na tofauti kimofofonolojia. Visawe vya nomino na vitenzi vimetambulishwa na sheria zinazosababisha utofauti kufafanuliwa kwa misingi ya mifanyiko ya kifonolojia na kimofolojia. Misingi ya nadharia mbalimbali za fonolojia na mofolojia zilitumika kama mwongozo wa uchanganuzi wenyewe. Kitabu hiki kitawafaa wanafunzi na walimu wa lugha ya Kiswahili hasa katika ngazi ya Vyuo vikuu. Pia kitawafaa Wanaisimu Kihistoria, wale wanaoshughulikia elimu lahaja na wale wanaonuiwa kujifunza lugha ya Kimaasai. Ni nyongeza kwa tafiti chache za kiisimu za lugha za Nilo-Sahara zilizopo.

“Mofofonolojia Linganishi ya Lahaja za Wamaasai” ni kitabu kinachotoa mchango muhimu kwa taaluma ya Isimu ya Kiswahili na Lugha nyingine za Kiafrika. Kimejadili kwa kina masuala ya Fonolojia na Mofolojia ya Kimaasai na kitawanufaisha sana wanafunzi na wasomi wa lugha [Dkt Toboso Mahero, Mwenyekiti wa Idara ya Lugha na Elimu ya Fasihi, Chuo Kikuu Kishirikishi cha Alupe, Kenya].

Alexander Meitamei ni mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara, Kenya. Ana shahada ya B.Ed kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta na shahada za uzamili na uzamifu kutoka Chuo Kikuu cha Egerton. Amechapisha makala mbalimbali ya lugha, elimu na taaluma zingine. Mbali na kufunza, kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Idara ya Malalamishi ya Umma, Chuo Kikuu cha Maasai Mara.

1 review for Mofofonolojia Linganishi ya Lahaja za Kimaasai: Kenya na Tanzania

  1. Felix konongoi

    I like this book, i will recommend to my friends

Add a review

Your email address will not be published. Required fields are marked *