Siri ya Ushairi

Category:

Description

Diwani ya Siri ya Ushairi ni kitabu chenye manufaa makubwa  kwa walimu, wahadhiri na wanafunzi katika viwango nyote vya masomo.  Kitabu hiki kinapambanua kwa kina masuala ya ushairi yaliyo sehemu ya mitaala ya shule za upili pamoja na vyuo vikuu. Sura ya kumi ya kitabu hiki imebeba mkusanyiko wa mashairi ya kimapokeo na ya kimapinduzi yanayoangaza masuala yanayoathiri  jamii.  Mashairi haya yametumia mitindo anuwai ya kibunifu na yanawapa wahakiki fursa ya kutalii mitindo  mbalimbali ya kuwasilishia maudhui katika mashairi.

Dkt. Mahero B. Toboso ni mwalimu na mhadhiri wa Kiswahili wa miaka mingi. Alifundisha katika shule anuwai nchini Kenya kabla ya kuwa mhadiri wa chuo kikuu. Kama mwalimu, Toboso alitunga tamthilia na mashairi ambayo yaliigizwa katika tamasha za shule na vyuo nchini Kenya na kushinda tuzo kadhaa. Kwa sasa, Dkt Toboso ni Mtiva, Shule ya Elimu na Sanaa za Jamii, Chuo Kikuu cha Alupe. Dkt. Toboso pia ametunga kitabu cha sarufi, “Mitindo ya Lugha ya Kidijitali.” Sasa, anashughulikia mswada kuhusu Tamthilia, Sanaa ya Thieta na Drama na mkusanyiko wa Hadithi Fupi, ambayo itachapishwa hivi karibuni.

Mosol Kandagor ni Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Moi. Kitaaluma, Kandagor hujikita katika isimujamii, tafsiri na ukalimani. Vilevile, amewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Moi, mwalimu wa Kiswahili kwa muda mrefu katika Chuo cha Biblia cha Baringo na pia aliwahi kuhudumu kama Mwalimu Mkuu katika Shule ya Upili ya Ebenezer, mijini Kabarnet katika Kaunti ya Baringo. Kwa sasa Prof. Kandagor anahudumu kama Mtiva Mshiriki katika kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii katika Chuo Kikuu cha Moi. Aidha, ni Mhariri Mkuu wa “Journal of Kiswahili and Other African Languages” na “Jarida la CHAKAMA”. Pia, ni Mhariri Msaidizi wa “Jarida la Mwanga wa Lugha”. Kadhalika, yeye ni Katibu wa Chama cha Waandishi wa Kiswahili (CHAWAKI) na mwanabodi wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Siri ya Ushairi”

Your email address will not be published. Required fields are marked *