Uhakiki wa Uozo wa Jamii katika Riwaya za “Vipuli vya Figo” na “Siku Njema”

Category:

Description

Kitabu hiki ni tahakiki ya uozo wa jamii kama ulivyosawiriwa katika riwaya mbili: Siku Njema, iliyoandikwa ya Profesa Ken Walibora, na Vipuli vya Figo, iliyoandikwa na Profesa Emmanuel Mbogo. Mwandishi wa kitabu hiki ameonyesha aina anuwai za uozo unaowaathiri watu katika jamii kwa jumla. Kitabu hiki kimewalenga wasomaji wapenzi wa uadilifu katika viwango vya shule za upili, vyuo vikuu na hata washikadau katika uwanja wa dini. Msomaji wa kitabu hiki ataweza kuelewa kwa kina aina ya uozo hasa unaoendelezwa katika danguro na ambao taasisi mbalimbali za jamii huhofia kuutaja. Kimsingi, msomaji ataweza kupata mbinu na mitazamo ambayo inaweza kuhusishwa ili kuibua uwezekano wa kubadilisha na kuadilisha jamii. Mwandishi wa kitabu hiki amehusisha matumizi ya lugha ambayo si changamano na kwa hivyo msomaji yeyote yule ataweza kuupata ujumbe uliomo kwa njia ya moja kwa moja.

Pauline Ndave Wambua ni mzamifu katika Chuo Kikuu cha Maseno. Amefunza katika kiwango cha shule ya upili, pia ameshikilia wadhfa wa mhadhiri wa muda katika uwanja huo wa Kiswahili. Amewahi kuwa mhadhiri msaidizi wa muda katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara, Chuo Kikuu cha Mount Kenya, Chuo Kikuu cha Moi na kwa sasa anatarajia kuukamilisha uzamifu hivi karibuni.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Uhakiki wa Uozo wa Jamii katika Riwaya za “Vipuli vya Figo” na “Siku Njema””

Your email address will not be published. Required fields are marked *